TANZANIA NA UTURUKI ZANUIA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI

Serikali ya Uturuki imeahidi kushirikiana na Tanzania kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii hapa nchini ikiwemo mapambano dhidi ya ukatili kwa Wanawake na watoto. Hayo yamebainishwa na Balozi wa Uturuki hapa nchini Dkt. Mehmet Gulluoglu alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu